
Leo usiku saa 3.30 kwa saa za Afrika ya Mashariki kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka baina ya miamba ya Ulaya kutokea Uingereza na Ujerumani.
Manchester City inayonolewa na Pep Gudiola itasafiri hadi katika viunga vya Allianze Arena mjini Munich Ujeremani kwa ajili ya kukipiga na Mabavarians timu ya zamani ya Gudiola.

Mchezo huo unaotegemewa kuwa mkali na kuna uwezekano mkubwa wakacheza vijana zaidi kwa kuwa wachezaji wengi wazoefu wapo mapumzikoni baada ya michuano ya Copa America na ile ya Euro iliyomalizika hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni