MCHEZAJI
MPYA wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amejibu mapigo vizuri kwa
Lejendari wa Klabu hiyo Eric Cantona ambae alidai ‘Kutakuwa na Mfalme
Mmoja tu wa Manchester!’.
Malumbano
hayo ya Mastaa Wawili hawa yalianza mara tu baada ya kuthibitika kuwa
Ibrahimovic amesaini Man United na Cantona, ambae alipachikwa Jina la
‘Mfalme’ wakati akiichezea Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kumtumia
Staa huyo wa Sweden ujumbe wa Video uliosomeka: “Nina ujumbe binafsi kwa
Zlatan. Umeamua kuwa United na huo ni uamuzi sahihi ambao umewahi
kufanya. Lakini kitu kimoja cha mwisho, kwa Manchester Mfalme ni mmoja
tu. Unaweza kuwa Mwana wa Mfalme na Jezi Namba 7 ni yako ukiipenda. Ni
zawadi yangu kwa kukukaribisha wewe. Mfalme ameondoka, Ishi Maisha
Marefu Mwana wa Mfalme!”
Ibrahimovic,
mwenye Miaka 34, akiongea na Gazeti la kwao Sweden, Aftonbladet,
alisema: “Namhusudu Cantona na nimesikia alichosema. Lakini sitakuwa
Mfalme wa Manchester. Nitakuwa Mungu wa Manchester!”
Kauli
hiyo, ambayo ilichukuliwa ni ya dhihaka, ilitolewa na Ibrahimovic
wakati yuko Vakesheni huko Marekani na anatarajiwa kwenda Jijini
Manchester Wiki hii kuanza rasmi Mazoezi na Wachezaji wenzake kwa ajili
ya Msimu mpya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni