
Klabu ya Simba leo imeadhimisha miaka 80 kwa furaha baada ya kupata ushindi dhidi ya AFC Leoprds ya Kenya waliokuwa waalikwa katika maadhimisho hayo.

Magoli mawili ya Ibrahimu Ajibu pamoja na moja la Shiza Kichuya yaliifanya Simba kuwa na goli 3 kabla ya dakika ya 65 huku Mrundi Laudit Mavugo akufunga goli la 4.
Hadi mwisho wa mchezo huo Simba waliibuka videdea kwa magoli manne kwa bila

Mchezo pamoja na kuwa maalumu kwa kuadhimisha miaka 80 lakini pia ulikuwa maalumu kwa kuwatambukisha wachezaji wapya hasa waliosajiliwa ambao ni pamoja na Laudit Mavugo, Method Mwanjali, Javier Bukungu, Shiza Kichuya, Mdhamiru Yasin, Mohamed Ibrahim, Jamal Mnyate, Hamad Juma na wengine.
Mwanachama wa Klabu hiyo anayehitaji kuwekeza klabuni hapo Mohamed Dewj(Mo) naye pia alikuwepo uwanjani hapo na mgeni rasmi wa mchezo huo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mh. Paul Makonda.
Ligi kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 20 August 2016 na timu ya Simba inatarajiwa kufanya vizuri kutokana na usajili mkubwa ilioufanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni