Jumatano, Julai 20, 2016

DEMBA BA AVUNJIKA MKUU

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amevunjika mguu akiwa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Uchina
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba

Raia huyo wa SENEGAL mwenye umri wa miaka 31 alivunjwa mguu na beki wa timu pinzani katika mchezo wa ligi ya UCHINA siku ya JUMAPILI.

Ba ambaye anaichezea SHANGHAI SHENHUA aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG  mita chache kutoka kutika eneo la 18 na kuanguka chini na mguu wake kupinduka visivyo kawaida na kuvunjika.

Kocha wa klabu yake GREGORIO MANZANO ameonya kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka .

Ba aliwahi kuichezea West Ham, Newcastle na Chelsea zote katika ligi kuu ya Uingereza kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Uchina akitokea Uturuki katika klabu cha Besiktas katika uhamisho uliogharimu PAUNI MILIONI 12.

Ba anaongoza orodha ya wafungaji mabao Msimu huu akiwa tayari amepachika mabao 14 katika michezo 18 aliyoteremka diumbani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni