Kwa mujibu wa Ratiba ya
Ligi Kuu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana,July 19, 2016
michuano hiyo itaanza Agosti 20 kwa mechi saba kuchezwa kwenye viwanja tofauti,
ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga Agosti 17, mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi za ufunguzi za
Ligi Kuu Agosti 20, Simba SC watacheza na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni