
Kocha wa Man City Pep Gudiola amewachimba mkwara wachezaji wa kikosi chake watakaoonekana kuongezeka uzito kupita kiasi kuwa hawatofanya mazoezi na kikosi chake.
Gudiola ambaye ni muumini wa soka la pasi nyingi awali alilifanya hilo akiwa na vikosi vya F.C Barcelona na Bayern Munchen ambako alijizolea sifa kwa kunyakua mataji.
Kwa mujibu wa Gudiola yeye anaamini kabisa kuwa mchezaji mwenye uzito mkubwa hawezi kutimiza majukumu yake uwanjani kama anavyohitaji kocha.
Inasemekana kuna baadhi ya wachezaji (hawakutajwa) wamekuwa wakijiachia sana katika ulaji wa vyakula hasa vile vyenye sifa za kuongeza uzito vijulikanavyo kitaalamu kama "junk foods". Mmoja wa wachezaji aliyezungumzia suala hilo la wachezaji kuwa wazito ni beki wa Man City raia wa Ufaransa Gael Clich.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni