Ijumaa, Julai 15, 2016

HII YA WATANI LEO NGUMU....!


Kumekuwa na kawaida kila Yanga wanapocheza na timu kutoka nje ya nchi basi mashabiki wa watani wao yaani Simba hupendelea kununua na kuvaa jezi za timu pinzani inayocheza na Yanga lengo likiwa ni kuwaunga mkono wapinzani wa Yanga.

Sasa katika mechi ya leo kati ya Yanga na Medeama ya Ghana kutakuwa na ugumu kwa mashabiki wa Simba kwani inasemekana kuwa Medeama hutumia jezi zenye rangi ya njano ambazo ni sawa na rangi wanazotumia Yanga.

Tungoje tuone nini kitatokea kwani ni ukweli usiopingika kuwa mashabiki wa Simba hawana kawaida ya kuwaunga mkono wenzao Yanga na halikadhalika Yanga nao huwa hawawaungi mkono wenzao Simba hasa wanapokuwa wanacheza na timu kutoka nje ya nchi.

Mechi ya Yanga na Medeama itachezwa leo katika Uwanja mkuu wa Taifa na Yanga wanalazimika kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni