
Baada ya kikosi cha timu ya medeama kuwasili nchini kikitokea Ghana, kocha mkuu wa kikosi hicho prince Yaw Owusu, amefunguka kuwa anawajua vizuri wapinzani wake Yanga, hivyo ana uhakika wa ushindi,
.
"Naijua Yanga vizuri tu kwani miezi michache iliyopita nilikuwa hapa na kikosi cha Al Khartoum kwenye kagame, nikiwa kocha msaidizi huku kocha mkuu akiwa ni Kwesi Appiah.
.
"Lakini kwa wachezaji wangu wote hii ni mara yao ya kwanza kuja hapa, lakini tumejiandaa kwa mapambano ili kuondoka na pointi zote tatu ambazo ndiyo tunazihitaji kufikia malengo yetu hapo baadae kucheza nusu fainali," alisema Owusu.
.
Naye nahodha wa kikosi hicho Mohammed Muntari Tagoe ambaye ni kipa alisema, wamekuja kushindana na wale wanaowabeza basi wasubiri kuona kitakachotokea uwanjani.
Yanga na Medeama zitapambana leo katika Uwanja mkuu wa Taifa na mchezo huo unatarajiwa kuanza mnamo muda wa saa 10 jioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni