
KUCHANIKA kwa jamvi sio mwisho wa shughuli, msemo huu ulidhihirika wakati wa Fainali ya Euro 2016 uliozikutanisha wenyeji Ufaransa dhidi ya Ureno, ambayo awali haikupewa nafasi ya kubeba taji hilo.
Katika mchezo huo, dakika 24 tu, Ureno ilimpoteza staa wake muhimu na nahodha wa kikosi hicho Cristiano Ronaldo, ambaye alipata majeraha ya goti baada ya kuchezewa vibaya na kiungo wa Ufaransa, Dimitri Payet.

Vipimo vya awali vinaeleza kuwa nyota huyo anaweza kuwa nje ya soka kwa miezi minne au mitano wakati akiendelea na matibabu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni