
Kocha bora wa msimu wa 2015/16 na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania klabu ya Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm amesaini mkataba mwingine wa miaka miwili wa kuendelea kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa mara mbili mfululizo kwa misimu ya 2014/15 na 2015/16.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa Mholanzi huyo ulimalizika mwezi uliopita na kutokana na timu hiyo kukabiliwa na michuano ya kimataifa ilibidi kusubiria tukio hilo la kusaini mkataba mpya.
Kocha huyo amekuwa na mafanikio makubwa na klabu hiyo ya Yanga na ameiwezesha kutwaa taji la ligi kuu mara mbili mfululizo na kuifikisha hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni