
Meneja wa zamani wa Manchester United na Everton David Moyes atachukua nafasi ya Sam Allardyce Sunderland (Sun), Sunderland, ambao wanatafuta meneja wa saba katika kipindi cha miaka mitano wapo katika mazungumzo na Moyes, 53, ambaye alifukuzwa kazi Real Sociedad mwezi Novemba (Guardian)
Juventus wamekubali ombi la Paul Pogba, 23, kujiunga na Manchester United na timu hizo mbili zimekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 100 (L'Equipe), Manchester United wamekubaliana maslahi binafsi na Pogba, ambaye atasaini mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni 220,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi (Daily Mail), Manchester United watamlipa wakala wa Pogba, Mino Raiola, pauni milioni 18.4 kukamilisha uhamisho huo (Guardian), Manchester United pia wanatarajiwa kumsajili winga wa Brentford Joshua Bohui, 17, ambaye atasaini mkataba wa miaka mitatu (Manchester Evening News)
Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Schalke, Leroy Sane, 20, kwa pauni milioni 42, na kwa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki katika mkataba wa miaka mitano (Sun), Pep Guardiola pia anataka kumsajili kiungo wa Real Madrid Toni Kross, 26.
Chelsea wamekataa dau la pauni milioni 14.25 kutoka Borussia Monchengladbach la kumtaka beki Andreas Christensen, 20, ambaye anaichezea klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopo (Daily Mail), wakati huohuo Chelsea wanaamini wamefanikiwa kumzuia Diego Costa, 27, asiondoke, licha ya jitihada za Atletico Madrid kumtaka. Chelsea pia huenda wakamfuatilia beki wa Benfica Victor Lindelof, 22 (Daily Star), meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema huenda akapanda dau jingine kumtaka mshambuliaji Alvaro Morata, 23, baada ya Real Madrid kukataa dau la pauni milioni 62.7. Chelsea pia wanafikiria kumrejesha Romelu Lukaku, 23, kutoka Everton (Daily Mail)

Dau la Newcastle la pauni milioni 5.5 limekubaliwa na Blackburn la kumsajili beki wa kati Grant Hanley, 24 (Chronicle), wakati huohuo kiungo wa Newcastle Georginio Wijnaldum, 25, anakaribia kuhamia Liverpool kwa pauni milioni 25 (Sunderland Echo)
Arsenal nao wameingia katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko, 26 (TalkSport)
Swansea wametoa dau la zaidi ya pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Tottenham Nacer Chadli, 26 (Times), hata hivyo Spurs wanasema thamani ya Chadli ni pauni milioni 15 (Daily Mirror)
West Brom wameongeza dau kufikia pauni milioni 10 kumtaka beki wa Leicester Jeffrey Schlupp, 23, baada ya pauni milioni 9 kukataliwa (Birmingham Mail)
West Brom bado hawajajibu dau la pauni milioni 20 la Stoke kumtaka Saido Berahino, 22 (Sky Sports
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni