
Yanga imeshindwa tena kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na timu ya MEDEAMA kutoka Ghana katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika uliochezwa leo jijini Dar es Salaam.
Yanga iliuanza mchezo kwa kasi sana kwani dakika ya 2 ya mchezo ilipata bao lake kupitia kwa Donald Dombo Ngoma aliyetulia baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mzimbabwe mwenzake Thaban Kamusoko.
Medeama walitulia na kunako dakika ya 17 walisawazisha kupitia kwa Donald Danso baada ya mabeki wa Yanga kujisahau.
Amissi Tambwe nusura aipatie Yanga bao la pili lakini hakuwa makini kumalizia baada ya kubaki peke yake na Golikipa wa Medeama.
Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Oscar Joshua na Amissi Tambwe na nafasi zao zikachukuliwa na Haruna Niyonzima pamoja na Juma Mahadhi, mabadiliko hayo hayakubadilisha matokeo ya mchezo japo ziliongezwa dakika 5 za ziada.
Kwa sare hiyo Yanga imejiweka pabaya katika kumaliza nafasi mbili za juu kwenye kundi lake kwani ina pointi 1 tu hadi sasa baada ya kucheza michezo mitatu.
Michezo iliyobaki kwa Yanga ni mitatu lakini ni mchezo dhidi ya MO BEJAIA ya Algeria pekee ambapo Yanga watachezea nyumbani. Mechi zingine ni dhidi ya Medeama utakaochezwa Takoradi nchini na ule wa Tp Mazembe mjini Lubumbashi nchini Kongo.
Takwimu za mchezo wa leo ni kama zinavyoonekana hapa chini

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni