Jumamosi, Julai 16, 2016

DEAL DONE: KANTE ATUA CHELSEA


Chelsea imekamilisha dili la usajili wa kiungo raia wa Ufaransa Ng'olo Kante aliyekuwa akikipiga na mabingwa wa EPL 2015/16 Leicester City.

Uhamisho huo umewagharimu Chelsea kiasi cha £32 na wamempatia mkataba wa miaka mitano.

Kiungo huyo alifanya vizuri msimu uliopita na kuisadia timu yake kutwaa ndoo ya EPL kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa na kufanya timu nyingi vigogo kummezea mate lakini ni Chelsea pekee ndiyo waliofanikiwa kupata saini ya Mfaransa huyo.

Klabu ya Leicester City ilimpata Kante kwa £5.2 na wamemuuza kwa faida kubwa ya £32.

Karibu Kante Darajani...!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni