Jana,
Jumanne timu ya Yanga ilishuka uwanjani kupambana na Medeama katika
mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika kwenye
Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi nchini Ghana.
Hata
hivyo, wachezaji baadhi wa Yanga wameipigia saluti Medeama kwa fitna
kabambe ilizowafanyia wakati walipotua Ghana kwa ajili ya mchezo huo
ambazo zilifanya waingiwe na hofu kubwa ya kutekwa walipokuwa njiani
wakitokea Accra kwenda Sekondi.
Wakizungumza
na Championi Jumatano kwa nyakati tofauti wachezaji hao ambao ni, kipa
Deogratius Munishi na mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe
walidai kuwa baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Accra, ilikuwa ni usiku na walijua kutoka hapo kwenda Sekondi wangepewa
ulinzi kutokana na umbali ambao wangesafiri kwa basi.
“Hata
hivyo, hali haikuwa kama tulivyotarajia, tulisafiri usiku huo kwa basi
tena kwa zaidi ya saa tano bila ya kuwa na ulinzi wa aina yoyote, hakika
kila mtu ndani ya basi alikuwa akimwomba Mungu kila tulipokuwa
tukifikiria hali ya usalama katika mataifa haya ya Magharibi.
“Akili
zetu zilitawaliwa na hofu kubwa kwani tulikuwa tukipita sehemu nyingine
zilikuwa ni mapori, hata hivyo hofu hiyo ilishuka baada ya kufika
Sekondi na ndipo tulipoanza kutaniana huku baadhi yetu tukiona hali hiyo
kama bonge la fitina ambalo wapinzani wetu walitufanyia kwa sababu
walituvuruga kwa kiwango kikubwa,” alisema Dida.
Kwa
upande wa Tambwe alisema: “Ilikuwa ni balaa tulifika tumechoka sana na
hakuna mtu aliyekuwa akiamini kama tutafika salama Sekondi kutoka Accra
ila tunamshukuru Mungu kwa hilo ila jamaa nimewakubali kwa fitna hiyo ya
soka."
SOURCE: CHAMPIONI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni