Kama
wanatania, lakini Prisons wapo ‘siriaz’ baada ya kocha wao, Abdul
Mingange kutamka wazi kuwa malengo yao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara
ni kuwa mabingwa na si kingine.
Mingange
amepewa mkataba wa miezi sita ya kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya
Salum Mayanga aliyetimkia Mtibwa Sugar. Msimu uliopita timu hiyo
ilimaliza ligi ikiwa ya nne huku Yanga wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa
ligi hiyo.
Mingange
alisema kila timu huwa na malengo ya kumaliza msimu ikiwa bingwa, hivyo
hata wao wana malengo hayo na wanaamini watafanikiwa kwa hilo.
“Tupo
kwenye maandalizi makali kuhakikisha tunafanya vizuri msimu ujao,
malengo yetu ni kuwa mabingwa kwani kama timu msimu uliopita ilimaliza
nafasi ya nne basi msimu ujao tunaweza kuwa mabingwa.
“Hayo
ni malengo kwa kila timu na ndiyo maana sisi pia tumejiwekea hivyo,
lakini pia nishukuru tu nimekuta kikosi kwenye hali nzuri na kwa hapa
kilivyo sina haja tena ya kuongeza mchezaji, waliopo wanatosha kuipa
timu ubingwa,” alisema Mingange ambaye aliwahi kuzinoa Mbeya City na
Ndanda kwa vipindi tofauti
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni