Jumapili, Agosti 07, 2016

LEICESTER vs MAN UNITED KUFUNGUA EPL LEO


Ligi kuu ya England inatarajiwa kufunguliwa rasmi leo kwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Mabingwa watetezi Leicester City na Mabingwa wa FA timu ya Manchester United.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Wembley utaanza mnamo saa 12.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki unawakutanisha magwiji wa Ukocha ambapo kwa Leicester City wanae Claudio Ranieri ambaye anataka kuonyesha kuwa msimu uliopita hakuchukua ubingwa kwa kubahatisha.

Kwa upande wa United wana kocha mpya ambaye ni bingwa wa maneno mengi na kocha wa zamani wa FC Porto, Inter Milan, Real Madrid na Chelsea Jose Mourinho akiwa na mchezaji wake anayetarajiwa kutamba Zlatan Ibrahimovic.

Kuchezwa kwa mchezo huo ni kiashiria kwamba ligi inaenda kuanza ambapo inatarajiwa kuanza wiki inayofuata.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni