Jumamosi, Agosti 06, 2016

MANJI AICHUKUA YANGA KWA MIAKA 10


Katika kile kilichoonekana kukata kiu ya wapenda soka nchini hususani mashabiki wa Yanga, leo mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amekabidhiwa rasmi kuiendesha timu hiyo kwa muda wa miaka kumi.

Hayo yamejiri leo katika mkutano wa dharura na wanachama wa Yanga kuamua kumkabidhi Manji timu na mapato yote yatakayopatikana yeye atakuwa akichukua 75% na 25% zilizobakia zitabakia kwa klabu.

Suala hilo limekuja na likafanywa haraka haraka ili kuwatangulia watani zao Simba ambao wanahubiri mfumo wa mabadiliko wakiwa wanasuasua lakini Yanga wamelifanya hilo kwa vitendo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni