Jumapili, Septemba 11, 2016

MTIBWA YATAFUNWA NA SIMBA. MAVUGO HUYOOOO.....!


Klabu ya soka ya wakata miwa ya MTIBWA leo imebugizwa magoli mawili bila majibu na Simba katika mchezo uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Uhuru.

Milango ilikuwa migumu kwa timu zote mbili katika kipindi chote cha kwanza kwani timu zote hazikuweza kufungana hadi mapumziko.

Ilionekana kuwa kipindi cha kwanza Mtibwa walikuwa hawataki kwenda mbele zaidi hali uliyoifanya Simba ishindwe kufunga, lakini kipindi cha pili Mtibwa walianza kufunguka kwenda mbele na kuifanya Simba icheze vizuri na alikuwa Ibrahim Ajib aliyeifungia Simba goli la kwanza kisha goli la pili likawekwa kimiani na Supastaa wa Burundi Laudit Mavugo.

Hadi mwisho wa mchezo Simba 2 Mtibwa 0.

Katika Uwanja wa Sokoine kule Mbeya, timu ya Toto African imechapwa bao 1 na timu ya Prison.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni