
Ukija Dar unapigwa 3 na Yanga, huo ndo msemo unaoweza kuusema kwa sasa kuhusiana na mechi ambazo Yanga imecheza ikiwa katika viwanja vya Dar es Salaam kwani katika mechi mbili ilizocheza Dar imeweza kushinda mechi zote kwa goli 3 kila mchezo.
Mechi ya leo jumamosi Septemba 10 Yanga imeifunga timu ya Majimaji kwa goli 3 bila, magoli yakifungwa na Deus Kaseke pamoja na Amissi Tambwe aliyefunga magoli mawili.
Katika mchezo huo Simon alikosa penati baada ya kugonga mwamba lakini jitihada za Deus Keseke aliimalizia penati hiyo baada ya kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Hadi mapumziko Yanga walienda katika vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wanaongoza kwa goli moja. Kipindi cha pili Yanga walikuja kwa kasi hadi dakika ya 79 Tambwe akagongelea msumari wa pili na baada ya dakika chache baadae akapigilia msumari wa tatu na kuhitimisha safari ya Wanalizombe kulitembelea jiji la Paul Makonda.
Kesho katika Uwanja huo wa Uhuru Simba watawakaribisha wakata Miwa wa Mtibwa kutoka Manungu mkoani Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni