
Mshambuliaji raia wa Zimbabwe Bruce Kangwa amewasili leo kwa ajili kufanya majaribio ya kujiunga na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati klabu ya Azam F.C
Mchezaji huyo wa klabu ya Highlanders F.C ambayo hadi sasa ndiyo inayoongoza ligi ya Zimbabwe ameshafunga mabao saba hadi sasa ambapo ligi imesimama kwa ajili ya mapumziko baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika na yeye ndiye kinara wa mabao katika ligi.

Kangwa ana uwezo wa kucheza nafasi tatu uwanjani ambazo ni beki wa kushoto, winga wa kushoto na mshambuliaji na pia ameshaichezea mechi 20 timu yake ya Taifa na hadi sasa yupo katika orodha ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni