Jumanne, Julai 19, 2016

MAN U YATENGA £87MIL KUMNG'OA POGBA JUVE


Ripoti zinasema kwamba Manchester United wanajiandaa kutoa £87mil ili kutoa ofa kwa Juventus kwa ajili kumsajili kiungo ambaye ametawala sana vyombo vya habari kwenye tetesi za usajili kipindi hiki Paul Pogba.

Inasemekana kwamba Man U wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa na Pogba atakuwa akivuna £10.92mil kwa mwaka.

Paul Pogba inaaminika kuwa yupo tayari kutua Old Trafford na endapo uhamisho huo utafanikiwa basi kiungo huyo Mfaransa atakuwa ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa.

Ingia facebook kisha like page yetu ya "SOKA WADAU" ili upate habari za michezo mbichi kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni