Jumanne, Julai 19, 2016

BOCCO MAMBO MAGUMU KWA KOCHA MPYA AZAM F.C


Kocha mpya wa Azam FC, raia wa Hispania Zeben Hernandez, amemkataa mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu hiyo John Bocco, kwa kusema hana kiwango cha kuichezea timu hiyo.

Taarifa zilizopatikana zimedai uongozi wa timu hiyo ukiongozwa na mmiliki wa timu Yousof Bakhresa, wanataka kukutana na kocha Harnandez, ili kuzungumzia swala la mchezaji huyo ikiwezekana aendelee kufanya naye kazi hivyo hivyo pengine anaweza kumbadilisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni