Jumatatu, Julai 18, 2016

CHANONGO ATUA MTIBWA SUGAR



Mchezaji wa zamani wa Simba Haruna chanongo amekamilisha uhamisho wa kutoka stand United chama la Wana ya Shinyanga kwenda Mtibwa Sugar au maarufu wakata miwa wa Turiani Morogoro.

Usajili huo umekuja kufuatia taarifa zilizoenea kuwa Chanongo alisaini mkataba mpya katika klabu ya Stand United iliyobadilishwa kuwa kampuni, Baada ya sakata hilo la timu ya Stand kufika mbele zaidi na kuonekana kundi hilo la Kampuni halina mamlaka ya kuiendesha timu hiyo na halitambuliki kikatiba.

Chanongo amesaini mkataba wa miaka miwili na wakata miwa wa Mtibwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni