Jumatatu, Julai 18, 2016

Tetesi za Usajili Ulaya18 July, 2016


Wakala wa kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23, hajaweka matakwa kwa mchezaji huyo kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United, lakini pande zote mbili zinataka mkataba huo kukamilika mapema (Manchester Evening News), Pogba huenda akaamua kusalia Juventus, kwa kuwa timu hiyo inacheza Klabu Bingwa Ulaya, huku Manchester United wakiwa kwenye Europa League (Times.

Manchester United wanafikiria kumsajili kiungo wa Liverpool Joe Allen, 26, ingawa mchezaji huyo ni kipaumbele kwa meneja wa Swansea Francesco Guidolin (South Wales Evening Post), Liverpool pia wanamfuatilia kiungo wa Newcastle Georginio Wijnaldum, 25, wakiwa wanataka kulipa pauni milioni 20 (Telegraph).


Everton watamchukua winga wa zamani wa Manchester United Jordi Cruyff kuwa mkurugenzi wa michezo, iwapo watashindwa kumpata Steve Walsh ambaye ni mkuu wa ajira wa Leicester City (Sun), kiungo wa Leicester Riyad Mahrez, 25, anajiandaa kuhamia kwa mabingwa wa Spain, Barcelona, baada ya kukataa mkataba mpya (Sun), hata hivyo meneja wa Leicester, Claudio Ranieri ana uhakika kuwa Mahrez haondoki King Power Stadium (Daily Star)


Roma imesema beki wake Kostas Manolas hauzwi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki, 24, amehusishwa na kuhamia Arsenal au Chelsea (Evening Standard)

Juventus wamewapa Manchester City beki wake Leonardo Bonucci, lakini klabu hiyo inataka pauni milioni 50 (Manchester Evening News).

Manchester City wako tayari kupambana na Manchester United kumsajili beki wa West Ham Reece Oxford, 17 (Sun).

Mshambuliaji wa West Ham Enner Valencia, 26, anasakwa na Swansea na pia Lazio, ingawa hawajaweza kulipa pauni milioni 15 (Daily Mirror)

Chelsea wanataka kumsajili kipa wa AC Milan Diego Lopez iwapo Asmir Begovic, 29, atajiunga na Everton (Gazza Mercato)

Meneja wa Stoke City Mark Hughes amesena Burnley hawatomsajili kiungo wake Charlie Adam, 30 (Burnley Express)

Southampton wataanza mazungumzo ya mkataba mpya na Cedric Soares, 24, baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango bora kwenye Euro 2016 akiwa na Ureno (Daily Mirror)

Tottenham wameanza mazungumzo na Marseille ya Ufaransa kutaka kumsajili winga Georges-Kevin N'Koudou, 21, kwa pauni milioni 11 (Daily Mail)

Barcelona na Real Madrid wanafikiria kumsajili kiungo kutoka Ureno, Andre Gomes, 22, ambaye klabu yake ya Valencia imesema ana thamani ya pauni milioni 54 (Super Deporte).

Ingia facebook kisha like page yetu ya "SOKA WADAU" kwa habari mbichi kabisa za michezo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni