Jumanne, Julai 26, 2016

HAWAJAWAHI KUSHINDA TANGU WAANZE KUVAA JEZI ZA MANJI


Timu ya Yanga leo imepokea kipigo kitakatifu nchini Ghana kutoka kwa timu ya Medeama Sc baada ya kufungwa goli 3 - 1

Yanga ilipata bao la kufutia machozi kwa njia ya penati iliyopigwa kiufundi na Saimon Msuva.

Ikumbukwe kuwa Yanga tangu imeanza kutumia jezi zenye nembo ya QUALITY GROUP haijawahi kushinda mechi yoyote. Imecheza mechi nne imefungwa mechi tatu na kutoka sare mchezo mmoja.


Tarehe 17 August ni mechi ya ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam, tuwasubiri Yanga watakavyotesa katika mashindano ya hapa Tanzania!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni