Jumatatu, Julai 18, 2016

REICESTER CITY KUMUWEKA SOKONI MAHREZ


Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City huenda wakamuweka sokoni kiungo wao kutoka nchini Algeria, Riyad Mahrez baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya. Leicester City tayari wameshakamilisha mpango wa kumuuza kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante ambaye mwishoni mwa juma lililopita alijiunga na Chelsea, baada ya kugoma kusaini mkataba mpya. Suala la kugoma kwa Mahrez kwa kigezo cha kutoridhishwa na mshahara wa Pauni 100,000 kwa juma, ufumbuzi wake unatarajiwa kutatuliwa na mpango wa kumuweka sokoni ili kusaka pesa ambazo zitatumika kumsajili mbadala wake huko King Power Stadium.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni