Jumatano, Julai 20, 2016

TAMBWE AELEZEA UKWELI KUHUSU BIFU LAKE NA NGOMA


MSHAMBULIAJI wa Yanga na mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita, Amiss Tambwe, amesema hawana tena ugomvi na mshambuliaji mwenzake Donald Ngoma.


Tambwe na Ngoma inadaiwa waliingia kwenye 'bifu' mwishoni mwa ligi na kupelekea wachezaji hao kutwangana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tambwe, alikiri kuwa na tofauti na mchezaji huyo lakini kwa sasa wameyamaliza.

"Tulikwaruzana na hili ni jambo la kawaida kwa wachezaji, lakini mwisho wa siku tumeyamaliza. Hatuna tena tofauti," alisema Tambwe.

Katika hatua nyingine, Tambwe alisema kuwa kocha wake, Hans van Pluijm huwa anamchezesha tofauti na alipokuwa akicheza Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni