
Lile sekeseke kati ya klabu ya Yanga na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kuhusiana na suala la mapato, jana
liliendelea na kuzua tafrani kubwa.
Ishu hiyo ilizuka mara baada ya mechi
kati ya Yanga dhidi ya Medeama kwisha
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Baada ya hapo, fedha zilihesabiwa na
lilipofikia suala la mgawo, uongozi wa
Yanga ulikubali lakini kwa sharti moja,
kutoa hundi na si fedha taslimu.
Yanga walisema wameamua fedha zote
ziende benki na usiku huo wangezikabidhi
kwenye kampuni ya ulinzi, kesho jumatatu
zingepelekwa benki na baada ya hapo,
mgawo ungepitia mfumo wa hundi.
Kwa kuwa hilo halijazoeleka, TFF
iliendelea kusisitiza kwamba watu
wapewe mgao wao "cash cash" kama
ilivyozoeleka, Yanga wakashikilia
msimamo wao. Suala hilo baadaye liliamuliwa na Serikali
na inaelezwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye alitaka zisigawiwe ili kuwe na
utaratibu sahihi.
Hali hiyo ilisitisha malumbano lakini
inaonekana TFF ilikwazika kupita kiasi
kutokana na Yanga kuanzisha utaratibu
huo.
Lakini upande wa Yanga, ulijieleza
kwamba umepanga kufanya hivyo ili
kutumia mashine za EFD wakati wa
malipo na itatoa lisiti kwa kila
watakaolipwa.

Kabla ya mechi ya Medeama, kulikuwa na
tafrani kubwa kati ya TFF na Yanga baada
ya klabu hiyo kuruhusu mashabiki kuingia
bure katika mechi ya TP Mazembe.
TFF iliambulia patupu, hali iliyofanya
kuandika barua kadhaa ikidai ilipwe huku ikikadiria idadi ya watu uwanjani, jambo
ambalo halikuwezekana.
Like page yetu facebook iitwayo "SOKA WADAU" ili uwe wa kwanza kupata habari za michezo zikiwa bado mbichi..!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni