Jumapili, Septemba 11, 2016

MTIBWA YATAFUNWA NA SIMBA. MAVUGO HUYOOOO.....!


Klabu ya soka ya wakata miwa ya MTIBWA leo imebugizwa magoli mawili bila majibu na Simba katika mchezo uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Uhuru.

Milango ilikuwa migumu kwa timu zote mbili katika kipindi chote cha kwanza kwani timu zote hazikuweza kufungana hadi mapumziko.

Ilionekana kuwa kipindi cha kwanza Mtibwa walikuwa hawataki kwenda mbele zaidi hali uliyoifanya Simba ishindwe kufunga, lakini kipindi cha pili Mtibwa walianza kufunguka kwenda mbele na kuifanya Simba icheze vizuri na alikuwa Ibrahim Ajib aliyeifungia Simba goli la kwanza kisha goli la pili likawekwa kimiani na Supastaa wa Burundi Laudit Mavugo.

Hadi mwisho wa mchezo Simba 2 Mtibwa 0.

Katika Uwanja wa Sokoine kule Mbeya, timu ya Toto African imechapwa bao 1 na timu ya Prison.

Jumamosi, Septemba 10, 2016

UKIJA DAR UNAPIGWA 3, TAMBWE AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI VPL 2016/17



Ukija Dar unapigwa 3 na Yanga, huo ndo msemo unaoweza kuusema kwa sasa kuhusiana na mechi ambazo Yanga imecheza ikiwa katika viwanja vya Dar es Salaam kwani katika mechi mbili ilizocheza Dar imeweza kushinda mechi zote kwa goli 3 kila mchezo.

Mechi ya leo jumamosi Septemba 10 Yanga imeifunga timu ya Majimaji kwa goli 3 bila, magoli yakifungwa na Deus Kaseke pamoja na Amissi Tambwe aliyefunga magoli mawili.

Katika mchezo huo Simon alikosa penati baada ya kugonga mwamba lakini jitihada za Deus Keseke aliimalizia penati hiyo baada ya kugonga mwamba na kurudi uwanjani.

Hadi mapumziko Yanga walienda katika vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wanaongoza kwa goli moja. Kipindi cha pili Yanga walikuja kwa kasi hadi dakika ya 79 Tambwe akagongelea msumari wa pili na baada ya dakika chache baadae akapigilia msumari wa tatu na kuhitimisha safari ya Wanalizombe kulitembelea jiji la Paul Makonda.

Kesho katika Uwanja huo wa Uhuru Simba watawakaribisha wakata Miwa wa Mtibwa kutoka Manungu mkoani Morogoro.

Jumamosi, Agosti 20, 2016

SIMBA YAANZA KUGAWA DOZI VPL


Simba Sc leo imeanza ligi vyema kwa kuitandika timu ya Ndanda goli 3 - 1 katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa.


Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji wageni Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya.

Katika michezo mingine Timu za Stand United na Mbao FC zimetoka sare ya kutofungana katika Uwanja wa CCM Kambarage - Shinyanga, wakata miwa wa Mtibwa wamepokea kichapo cha goli 1 kutoka kwa Ruvu Shooting ya Masau Bwire. Nao Prison wameshinda goli moja dhidi ya Majimaji kule Songea.

Jumatano, Agosti 17, 2016

BALE AREJEA UWANJANI MADRID YAPIGA 5



Winga wa Real Madrid ya Hispania, Gareth Bale akiwatoka wachezaji wa Stade-Reims katika mchezo wa kirafiki wa mwisho wa kujiandaa na msimu mpya wa La Liga. Real Madrid imeshinda 5-3 Uwanja wa Santiago Bernabeu mabao yake yakifungwa na Nacho, Sergio Ramos, Alvaro Morata, James Rodriguez na Mariano Diaz.

MANENO YA MANJI KUHUSU YANGA



" waambieni wana- Yanga pamoja na vurugu zote na kashfa ninazopewa lakini nitaendelea kuwa upande wao ,na kamwe sitawaacha kwani nguvu yangu kubwa ipo kwa wanachama , wapenzi na mashabiki wa Yanga Afrika"

Yusuf Manji.

NGAO YA JAMII, ANGALIA KIKOSI CHA YANGA LEO


NGAO YA JAMII | TZ BARA | 2016.
Young African SC Vs Azam FC.
Uwanja : Taifa.
Muda : Saa 10 : 00 alasiri.
Live On : ATN

KIKOSI CHA YANGA | LEO

1.Deogratius Bonaventura Munishi 'Dida'
2.Hassan Ramadhan Kessy 'Alves'
3.Haji Mwinyi Ngwali 'Marcelo'
4.Mbuyu Junior Twite 'Chuma'
5.Vincent Bossou 'Kaka Jambazi'.
6. Said Juma Makapu.
7. Haruna Niyonzima 'Fabregas'
8.Juma Mahadhi 'Neymar'.
9.Thaban Michael Kamusoko 'Fundi'
10.Amissi Jocelyn Tambwe
11.Donald Dombo Ngoma.

Akiba:
Benno Kakolanya
Oscar Joshua
Deus Kaseke
Simon Msuva
Malimi Busungu
Matheo Anthony
Pato Ngonyani.